-->

Aika: Nina Wivu Kabambe na Nahreel Acha Tu

Memba wa Kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale amefunguka kuwa ana wivu wa kupindukia kwa memba mwenzake ambaye ni mpenzi wake, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wanaotamba na wimbo wao wa Kamatia Chini kwani kuna kipindi huwa anapata wakati mgumu hasa warembo wanapokatiza mbele ya jamaa huyo.

navi

Aika aliliambia Wikienda kuwa kila mwanadamu ana moyo na kuna watu wengine wanaweza kuwaona kuwa wapo tu wala hawaoneani wivu lakini ukweli ni kwamba ana wivu na mpenzi wake huyo.
“Watu wanadhani sina wivu lakini ninao kinoma lakini nagugumia kimoyomoyo,” alisema Aika.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364