-->

Milioni 50 za Kayumba Zimeisha, Kanunua Gari -Fella

Meneja wa kundi la Yamoto Band na diwani wa kata ya Kirungule amefunguka na kusema kuwa Kayumba Juma mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS) amemaliza pesa yake milioni 50 na kusema katika vitu alivyofanyia pesa hiyo ni pamoja na kununua gari.

FELLA

Akizungumza kwenye eNEWS Said Fella amedai kuwa walimnunulia gari msanii huyo kutokana na kazi yake hiyo ya sanaa pamoja na jinsi ambavyo jamii inamchukulia msanii huyo hivyo uamuzi wa kumnunulia gari ulikuwa ni uamuzi sahihi.

“Kwa pesa alizopata Kayumba zile milioni 50 amenunua gari na zingine amejenga hilo banda au nyumba ndiyo maana hata hiyo finishing ya nyumba atafanya baada ya kuanza kupata show, ila zile milioni 50 ziliisha. Mwisho wa siku anajenga nyumba kwa hela yake siyo kujenga nyumba kwa hela aliyotunzwa na mtu, kwa hiyo lazima sanaa yake imsababishie kujenga nyumba inayofanana na yeye na maisha yake”. alisema Said Fella

“Tukisema kwanini alinunua gari na si kujenga nyumba hilo nalo ni kosa yule ni msanii hivyo angepanda daladala mngesema kuwa kwanini amepanda daladala unajua nyumba siku zote haionekani” alisisitiza Said Fella

Kayumba

Kayumba

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364