Ajiua Baada ya Kukamatwa na Viroba
Mfanyabiashara na muagizaji wa pombe za viroba, Festo Mselia, amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi ikiwa ni siku moja baada ya jeshi la polisi kuendesha msako na kukamata shehena ya pombe katika ghala alililokuwa akilimiki mjini Dodoma.
Katika vita ya kupambana na matumizi ya pombe za vifungashio aina ya viroba vilivyopigwa marufuku, jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata shehena hiyo ya katoni 1,400 ikiwa na thamani ya shilingi bilioni moja katika ghala la mfanyabiashara huyo.
Mfanyabiashara huyo aliyejiua ni wakala mkuu wa uagizaji na usambazaji wa pombe hizo akiwa anamiliki ‘store’ ya Mselia Intapreses.
Awali katika msako huo ulioongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, alimtaka mfanyabiashara huyo kuendelea na shughuli zake, huku akiamuru shehena hiyo isiuzwe wala kutumika wakati akisubiri maelekezo mengine.
Mambosasa amesema jeshi linaendelea na uchunguzi kabla ua kutoa taarifa rasmi.
eatv.tv