-->

DUMA: Ninayo Siri ya Kuikomboa Bongo Muvi

MSANII wa filamu anayepanda kwa kasi Bongo, Daud Michael ‘Duma,’ amesema anaifahamu siri inayowafelisha wasanii wengi Bongo siku hadi siku kiasi kwamba kwa sasa tasnia ya filamu inaonekana kupoteza mvuto. Akipiga stori na Uwazi Showbiz , Duma ambaye muda mwingi anapenda kuutumia kufanya mazoezi ya kazi zake za filamu, alifunguka kuwa kinachowafelisha wasanii wengi wa Bongo ni uvivu na kutopenda kujishughulisha na kufanya kazi kwa mazoea.

“Unajua siri iliyojifi cha nyuma ya kufeli kwa wasanii wa Bongo ni uvivu, hakuna cha zaidi, wasanii wengi ni wavivu, hawajishughulishi kabisa na hata kazi wanazofanya ni zilezile,” alisema Duma.

Mkali huyo aliyeibukia kupitia Tamthiliya ya Siri ya Mtungi aliendelea kusema kuwa kama wasanii wote wa fi lamu wangekuwa wanajituma kama ilivyokuwa kwa marehemu Steven Kanumba basi soko la filamu lingekuwa mbali nchini.

Duma akiwa lokesheni na baadhi ya wasanii na wadau wa Bongo Movi

Kwa upande wake alisema amejipanga kuhakikisha anapiga hatua zaidi katika fani hiyo ya kuuza sura kupitia runinga na kuongeza kuwa anatarajia kupeleka sokoni kazi nzuri zenye ubora wa kimataifa.

“Nataka nifuate nyayo za Kanumba, nicheze fi lamu safi  zenye ubora wa kimataifa na ambazo zitalisogeza mbele soko letu la fi lamu, Watanzania wakae mkao wa kula kupokea kazi nzuri kutoka kwangu ambazo zitaanza kutoka hivi karibuni,” alimaliza Duma.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364