Aliyedaiwa Kumbaka Shilole Afunguka Mazito!
KATIKA maho-jiano na Mwandishi nguli wa burudani nchini wa Gazeti la Ijumaa, Erick Evarist, Februari 2012, msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alinukuliwa akieleza kisa hiki:
“Katika maisha yangu nimepitia mitihani mingi, mmoja wapo ni huu wa kulazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yangu, kwa kifupi nilibakwa.”
Kwa kuwa kisa hiki cha kusikitisha kimesemwa sana na Shilole katika mahojiano yake mengi na vyombo mbalimbali vya habari, Gazeti la Ijumaa lililazimika kufunga safari mpaka wilayani Igunga mkoani Tabora ili kumtafuta anayetuhumiwa kumbaka ambapo lilifanikiwa kufanya naye mahojiano.
UTAMBULISHO WA JINA NA MAKAZI
“Kwa jina naitwa Makala Elia Joseph. Nimezaliwa mwaka 1988 ni mtoto wa pili katika familia yetu. Naishi hapa Igunga, karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Barabara ya Singida.
Mwandishi: Umejitambulisha vyema. Mimi ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Ijumaa, nimetoka Dar…(Kicheko kinakatisha maelezo).
Makala: Hahaha, umekuja kunihoji kuhusu Shilole? Dah! Ninyi ni watu hatari sana.
Mwandishi: Kwa nini Shilole na siyo mtu mwingine?
Makala: Niliposikia wewe ni mwandishi nilijua utakuwa unataka kunihoji kuhusu yeye, maana nasikia kwenye vyombo vya habari anatangaza kuwa nilimbaka, jambo hili linaniumiza kweli.
MAJIBU KUHUSU UBAKAJI
Mwandishi: Nashukuru kwa kufungua msingi wa mahojiano yetu, unaweza kueleza unafahamu nini kuhusu tuhuma za kubaka zinazoelekezwa kwako?
Makala: Mimi nimbake Shilole? Hebu zunguka tu hapa stendi, waulize watu kama kweli nilimbaka, niliishi naye kama mke wangu, watu wote wanajua.
Mwandishi: Wanaweza kuwa wanajua kuwa uliishi naye lakini wasijue kuwa ulimbaka. Maana inadaiwa kuwa ulikuwa na uhusiano naye tangu akiwa darasa la sita.
ZAMU YA KUSIKIA HISTORIA
Makala: Wakati anasoma hakuwa mpenzi wangu, alikuwa jirani yangu. Kutokana na maisha ya shida aliyokuwa nayo (Hali za wazazi wake zinaelezwa ambazo hazina sababu ya kuandikwa), nilikuwa namnunulia nguo na vifaa vya shule.
Mwandishi: Kwa hiyo ukaona utumie shida hizo kufanikisha mtego wako?
Makala: Siyo hivyo, nilikuwa namsaidia kama dada yangu, lakini baadaye alipomaliza shule pengine kwa kuridhishwa na mimi akaanza kunionea wivu, akawa anakuja chumbani kwangu mara kwa mara tunakaa bila kufanya chochote.
Mwandishi: Zungumzia suala la kubaka na wapi ulikutana naye kimwili kwa mara ya kwanza!
Makala: Ilikuwa chumbani kwangu, yeye ndiye ‘aliyefosi’ si unajua mtoto wa kike akikupenda anavyokuwa?
MAELEZO YA KUMPA MIMBA HAYA HAPA
Mwandishi: Katika mahojiano yake, Shilole anasema, ulipombaka ndiyo ulimpa ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.
Makala: Mtu utambaka kila siku? Nakuambia nilikuwa naye kwangu, ndugu zake waliniruhusu. Hiyo mimba nilimpa baada ya kuishi naye sana.
Mwandishi: Mlifunga ndoa? (Makala anajibu haraka kuwa hawakufunga na kwamba alikataa kumuoa kwa sababu aligomea sharti la kubadili dini ambapo aliruhusu swali kuendelea). Halafu Makala anaposema ulimbaka huenda ulitembea naye akiwa na umri mdogo!
Makala: Hakuwa mdogo (swali la miaka linaulizwa katikati) sijui alikuwa na miaka mingapi ila alikuwa mkubwa kabisa.
Mwandishi: Ilikuwaje mkaachana ilhali ulikabidhiwa na ndugu zake?
Makala: Baada ya kuzaa naye na kumuweka vizuri (anajisifu kumpigisha ‘pamba za nguvu’, vimini na raba za kijanja) kuna jamaa anaitwa Twaha, alikuwa dereva katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Dodoma – Singida alianza naye uhusiano.
Mwandishi: Wewe ulijuaje kuwa mpenzi wako kapata bwana mwingine?
Makala: Visa vilizidi na hawakuwa wakijificha; mwisho walioana kabisa. Hapo ndiyo ukawa mwisho wa mapenzi yetu.
Mwandishi: Una ujumbe gani kwa Shilole?
Makala: Asinizungumzie vibaya, mimi ni mzazi mwenzake, akumbuke wema wangu, ‘asinidisi’ kwenye vyombo vya habari, watu wanaomjua wanamshangaa.
Mwandishi: Swali la kachumbari; vipi Shilole mzuri kwenye mambo fulani ya kikubwa?
Makala: (Kicheko sana) Siwezi kumponda.