-->

Mpoto, Muhogo Mchungu Wahimiza Usomaji wa Vitabu

mpoto, muhogo mucungu

WASANII wa fani mbalimbali wametoa wito kwa wananchi na wanafunzi kuwa na desturi ya kujisomea vitabu vya lugha ya Kiswahili ambavyo vitawasaidia kukuza lugha hiyo.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa kitabu cha fasihi cha ‘Mwele bin taabani’, kilichoandikwa na aliyekuwa Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir, msanii Mrisho Mpoto alisema kuwa kama Watanzania wanahitaji lugha hiyo kuthaminiwa lazima wahakikishe wanaithamini.

“Ni vigumu lugha kuthaminiwa na wageni wakati wenyeji wa lugha husika hawaithamini na njia mojawapo ya kuithamini ni kusoma vitabu vya fasihi ambavyo vinaandikwa na watunzi mahiri kama akina Mudhihir ambaye kwangu namuona kama ‘Chinua Achebe’,” alisema Mpoto.

Naye mwigizaji, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’ na mchora katuni mashuhuri, Masoud Kipanya, walitoa wito kwa wananchi kujisomea vitabu vya aina hiyo, ikiwamo na serikali kuvitumia kwenye mitaala yake ya elimu ya sekondari na vyuo.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364