-->

Amanda Asubiri Ndoa Amuanike Hubby Wake

Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa amejifunza kuwa msiri kwenye uhusiano wa kimapenzi na sasa atamuanika mpenzi wake atakapokaribia kufunga ndoa.

amanda34

Akipiga stori na Ijumaa Amanda alisema kuwa, siku hizi amekuwa hapendi kuweka wazi kajiweka kwa mwanaume gani kutokana na historia ya maisha yake ilivyoathirika kwa kujianika.

“Yaani mtu akiniuliza  kuhusiana na mahusiano yangu anakuwa ananichokoza kwa sababu sipo tayari kuyaanika tena na sitakaa nikaongelea tena kuhusu maisha yangu ya kimapenzi yaliyopita wala ya sasa. Kumuanika hubby wangu ni mpaka ndoa,” alisema Amanda.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364