-->

Mr. Blue Amshushia Lawama Sugu, Kisa Wimbo

Msanii Mr. Blue amelalamikia kitendo cha msanii mwenzake ambaye pia ni mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi au Mr. Sugu, kwa kuchukua wimbo aliomshirikisha na kuufanya wake bila ridhaa yake.

Sugu

Kwenye ukurasa wake wa instagram Mr. Blue ameandika ujumbe huku akiomba mashabiki wake wamshauri nini afanye, kwani Mr. Sugu anamheshimu kama kaka yake.

“Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa Makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu, je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu….????”, aliandika Mr. Blue.

Wimbo huo wa ‘Freedom’ ambao tayari upo kwenye mitandao, umeonekana ukiandikwa ni Mr. Blue ft Sugu, huku mwingine ambao umeshafanyiwa video unaonekana ukiandikwa wa Sugu ft Lizzy.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364