Amanda Atumika kwa Utapeli
Kaa chonjo! Staa wa Bongo Movies, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya jina lake kutumika kwa utapeli kwenye mitandao ya kijamii.
Amanda ameliambia Ijumaa Wikienda kwamba, kuna Amanda feki anayetumia jina lake kutapeli watu ambapo tayari amepokea malalamiko mengi huku jamaa mmoja akichukuliwa fedha kilaini (hakutaja kiasi) kupitia Facebook, akiamini ni staa huyo hivyo kuwataka watu kuwa makini kwani yeye hana mchezo huo.
Chanzo: GPL