-->

Amini Amenibadilisha Kimuziki – Peter Msechu

Msanii Peter Msechu amefunguka na kusema kuwa yeye saizi kuanza kufanya vizuri kwenye muziki ni kutokana na kufanya collabo na baadhi ya wasanii kama Amini na amekiri wazi kuwa Amini ndiye ameweza kumfanya atambue watanzania wanapenda nini.

Peter Msechu6

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Peter Msechu amesema kuwa mafanikio ya yeye kuanza kufanya vizuri kwenye muziki ni baada ya kuweza kukamilisha Collabo yake na msanii Amini inayoitwa ‘Nyota’.

“Unajua kwa sasa mimi naweza kusema Collabo sasa basi maana nimefanya sana kazi kwa kushirikiana na watu na kiukweli kwenye Collabo mimi nilikuwa natafuta njia. Amini amenisaidia sana mimi kwani kuna wakati nilikuwa nikienda studio nilikuwa napenda kufanya muziki fulani mgumu yaani nilikuwa nafanya muziki kitaalamu. Na weka masauti magumu ambayo hata yalikuwa hayana na maana yoyote ndiyo Amini akaniambia Msechu watanzania hawataki hayo mambo, watanzania wanataka muziki usio na ufundi sana ndiyo maana baada ya kubadilika nikafanya wakanipokea vizuri” Alisema Peter Msechu.

Kufuatia jambo hilo Peter Msechu amedai kwa sasa tayari ameshafahamu njia ya muziki ambayo watanzania wanataka hivyo ni wakati wake kuja na kazi akiwa yeye mwenywe bila kutegema tena Collabo kama ilivyokuwa awali.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364