-->

AMINI Atoboa Kile Kinacho Sababisha Wasanii Wengi Kuingia Kwenye Utumia wa Madawa ya Kulevya

ALIYEWAHI kuwa mchumba wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Linah Sanga, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’ amesema makundi mabaya wanayokuwa nayo baadhi ya wasanii ndiyo yanayowaingiza katika matumizi ya dawa za kulevya

amini34

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Hawajui’ alisema wasanii wengi hawajitambui kutokana na makundi waliyonayo, ndiyo maana hushindwa kusimamia hata kazi zao za muziki kiasi cha kukosa mwelekeo.

“Tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii nchini linaonyesha kuondoa taifa linalohitajika nchini katika kusaidia ukuaji wa uchumi wake, hivyo inabidi waachane na makundi yasiyo na mwelekeo,’’ alisema.

Dawa za kulevya kwa wasanii limekuwa janga baada ya wasanii wenye majina makubwa kukamatwa na kufungwa katika magereza ya nchi mbalimbali na baadhi yao kupatiwa huduma katika baadhi ya vituo vya kusaidia kuachana na matumizi hayo.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364