-->

Wema Sepetu Akutana na Lema, Afunguka Maneno Haya

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye hivi sasa amehamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametimiza hadi yake kwenda kuonana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema ambaye amepata dhamani siku ya Ijumaa na kutoka gerezani.

Wema Sepetu juzi alisema atakwenda Arusha kuonana na Mbunge huyo ambaye amekaa ndani kwa zaidi ya miezi mitatu na kusema ni faraja kwao saizi kuona ametoka na kuja kuendeleza mapambano

“Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano, kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho (jana) i’ll be in Arusha kuonyesha Solidarity” alisema Wema Sepetu

Baada ya Wema Sepetu kufanikiwa kuonana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema amefunguka na kusema saizi anajisikia furaha na amani kuwa ndani ya chama hicho

“Finally Met my brother, aisee Chadema inanipa furaha mimi. Nina amani ya moyo… Ona Venye nacheka …. It was A Good Day….” aliandika Wema Sepetu

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364