-->

Baada ya Kuokoka, Kajala Akejeliwa

BAADA ya kukiri katika gazeti hili kuwa ameamua kuokoka na kumrudia Mungu, mrembo kunako filamu za Kibongo, Kajala Masanja amekejeliwa na baadhi ya watu wake wa karibu.

KAJALA623

Akizungumza na Amani Kajala alisema kitendo cha kuokoka kimegeuka kama kejeli kwa marafiki zake ambapo wengi humcheka lakini anaamini kabisa siyo akili zao bali shetani anataka kuwatumia ili aanguke.

“Kuna ambao wananicheka kicheko kikubwa kabisa baada ya kusikia kuwa nimeamua kumfuata Yesu na wengine kunikejeli lakini mimi sina neno naamini kabisa ni nguvu ya shetani ili nirudi nilikotoka, nawaambia tu watakuwa wamechelewa sana,” alisema Kajala.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364