-->

Tanzia: Muigizaji Kinyambe Afariki Dunia

Komediani aliyetamba kwa kubadilisha sura na sauti yake katika filamu za uchekeshaji nchini, James Peter Nsemwa a.k.a Kinyembe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Mohamed Abdallah a.k.a Kinyembe enzi za uhai wake

Mohamed Abdallah a.k.a Kinyembe enzi za uhai wake

Mpaka mauti yanamfika, Kinyambe alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Akiongea na EATV Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba, amesema ameongea na baba mzazi wa marehemu na kuthibitisha kifo hicho, ambacho kimesababishwa kwa ugonjwa wa mapafu kujaa maji.

Mwakifwamba amesema taratibu za mazishi zinaendelea mkoani Mbeya ambako ndio nyumbani kwao marehemu, na wanaangalia kama kuna uwezekano wa wasanii wenzake kuhudhuria.

RIP Kinyambe

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364