Baba Haji: Ni Mwendo wa Kutoa Vipaji Tu!
HAJI Adam ‘ Baba Haji’ anasema kuwa elimu yake ya Sanaa aliyosoma anaitumie kwa kuwasaidia wasanii wenzake na kuwatia moyo kuwa wana nafasi ya kuweza kujiunga na vyuo vya sanaa endepo watatenga muda na kujigawa kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kitaaluma.
“Nimekuwa mwalimu mzuri kila ninapokutana na wasanii chipukizi hata wakubwa kujaribu kuwagawia kile nilichojariwa kukipata nikiwa chuo cha Sanaa Bagamoyo na wengi wananishukru na nitaendelea kufanya hivyo,”Baba Haji
Baba Haji mwigizaji mahiri katika sinema za mahaba baada ya kumaliza Tasuba alijikita tena katika filamu akiwa ni muongozaji, mtayarishaji na kuigiza pia na amekuwa akitumia muda mwingi katika kufundisha vikundi vya sanaa katika mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.
FC