-->

Ommy Dimpozi Alinisumbua Sana- AliKiba

Msanii Alikiba amefunguka na kusema msanii Ommy Dimpoz alimsumbua sana ili kufanya naye ‘Collabo’ japo anasema alikuwa anamsumbua kwa namna nzuri na si mbaya kwani lengo lake lilikuwa ni kufanya kazi na yeye.

Alikiba akiwa na Ommy Dimpoz katika pozi

Alikiba akiwa na Ommy Dimpoz katika pozi

Akiongea na East Africa Radio Alikiba alidai kuwa ilimchukua takribani mwezi mmoja kama si miwili ili kufanya kazi hiyo na Ommy Dimpoz kwani anadai kila alipomuahidi kwenda studio mambo yaliingiliana na kujikuta inakwenda zaidi ya miezi miwili ndipo alipopata nafasi na kwenda studio kukamilisha Collabo hiyo.

“Ommy Dimpoz alikuja akaniambia Kaka kuna wimbo fulani nataka tufanye, mimi nikamuuliza wewe si unaimba kwenye band? akaniambia ni kweli ila kwa sasa nataka kutoka mwenyewe nikamwambia sawa. Nikamuuliza wimbo huo umefanya wapi akasema kwa KGT nikamwambia pale ni nyumbani kwangu, hivyo nikapata nafasi kuisikiliza kazi ile na kumwambia wimbo huu unahitaji vitu vya ziada. lakini ilinichukua zaidi ya mwezi kama si miezi miwili kwenda studio sababu mambo yalikuwa yanagingiliana lakini alikuwa akizidi kunisumbua si kwa nia mbaya au kwa ubaya ni vile mambo yangu yalikuwa mengi na yalikuwa yanaingiliana ila nakumbuka majibu yangu yalikuwa ya matumaini kwake” alisema Alikiba

Mbali na hilo Alikiba alitoa siri yeye kufanya kazi ambazo zinapendeka na mashabiki ni kwa sababu mara nyingi anapofanya kazi huwa anaangalia mashabiki zaidi na si kuangalia yeye ile kazi anaionaje, pia alisema katika ufanyaji kazi huwa anafanya kazi kwa kufuata hisia zake na si kukurupuka tu studio na kufanya kazi.

“Unajua mimi siku zote huwa nafanya kazi kwa ‘feelings’ hata nikiwa studio naweza nikakaa tu mpaka hisia zinijie ili nikifanya pale kazi watu waweze kuielewa” aliongeza Alikiba

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364