Young Killer Aizungumzia Picha Yake na Diamond
Picha aliyoiweka rapa Young Killer kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na Diamond, imezua maswali kadhaa ya matumaini miongoni mwa mashabiki wake.
Rapa huyo wa Mwanza amepost picha akiwa na Diamond Plutnumz na kuandika:
Hakuna mtu aliye zaliwa ili aje awe maskini (ndiyo ) unaweza ukawa umezaliwa kwenye familia maskini ila ukweli ni kwamba hujazaliwa ili wew uje kua maskini….hivyo bas ::mafanikio uja kwa wale walio shindwa mara nyingi na wakajaribu tena kwa ujasiri.. (yes) mungu nisaidie yatimie .. with MSAFI @diamondplatnumz
Baada ya post hiyo iliyoibua maswali mengi, Bongo5 ilimtafuta Young Killer na kuzungumzia swala hilo.
“Hakuna kitu chochote kinachoendelea, nimepost tu,” alisema Young Killer. “Kama ikitokea nimesaini mtasikia. WCB ni label kubwa na kila mtu anatamani kufanya nayo kazi, kwa hiyo ikitokea nikajiunga pale ni jambo la heri sana,”
Bongo 5