-->

Baraka Awaponda Wasichana Wanaomshobokea

Msanii Baraka da Prince amewapa za uso watu wanaomchafua kwa kusema kuwa wana mahusiano nae, na kusema jitihada zao za kumuharibia taswira yake kwenye jamii zimegonga mwamba.

new-bk-444

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Baraka amepost picha akiwa na mwananmke lakini hakumuonyesha sura ni nani, na kusema kuwa mwanamke huyo ndiye anayemtambua na sio wengine.

“My life na uyu tu ndio namtambua, hao mnawatambua ninyi, haya ni maisha yangu,na yapo kwenye serekali yangu, ustake niishi unavyotaka, mnajaribu sana kuchafua jina langu kwa mashabiki zangu, na pia mnajarbu kushusha heshima yangu kwa wanaonieshimu ila mmechelewa sana, nachoamini shabiki wa kweli awezi nichukia kwa upumbavu au uvumi wa kijinga unaoendelea, hii ya mtoto imegoma tengenezi nyingine tena,na tambueni haya ni maisha yangu #SUPER na tumeshamjua anaewatuma kunichafua”, aliandika Baraka da Prince.

Hivi karibuni Baraka alikanusha kuwa na mahusiano na msanii wa filamu za kibongo Nisher ambaye alikuwa anasema kuwa ni mpenzi wake, na kusema akuwa yeye ndio baby mama wake kwani ana ujauzito wake.

ali-kiba-na-jokate

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364