-->

Lowassa Bado Una Nafasi Kubwa Kwangu -Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini na aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa bado aliyekuwa mgombea wa urais nchini mwaka jana kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yupo moyoni mwake.

Shamsa Ford

Kupitia Account yake ya Instgram Shamsa Ford alipost picha ya Mh Edward Lowassa na kusema ni kumbukumbu yake lakini siku zote atakuwa na nafasi moyoni mwake.

“My FIRST TBT…YOU will always have a space in my heart dady…✌✌” Aliandika Shamsa Ford

Kipindi cha kampeni za uchaguzi Shamsa Ford alikuwa ni kati ya wasanii ambao walionyesha wazi kumpa support Mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA na aliyekuwa akiungwa mkono na UKAWA, Mh Edward Lowassa.

Lakini kutokana na post hiyo wapo baadhi ya mashabiki ambao walionyesha kutopenda ujumbe wake huo huku wengine wakimuunga mkono kwa kusema kuwa Edward Lowassa alistahili kuwa kiongozi wa juu wa nchi, kama ambayo Comment zinavyosema hapo chini.

“Miaka elfu moja haitatokea awe Rais labda awe Rais wako wewe Shamsa na Nay mibangi wako” Peterteddy31

“Huyo hatumtaki sasa hivi hapa ni kutumbua mijipu tu mabadiliko peleka Monduli maana tulichotaka tunakiona kwa Magufuli wewe huna jipya” Alisema Saidi_geleta

“Huyo ndio Mr president wangu hata wanune ukweli wanaujuaaa u winn” Alisema mc_nyemolicious

“Hapo nakupendaga sana Shamsa Ford, ni vizuri kuamini unachoamini ni sawa, na ni mbaya kumdhihaki mtu anachoamim” Alisema frankatilio

eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364