-->

Baraka, Najma Wagandana Kama Ruba

Mkali wa Ngoma ya Siwezi, Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’ amejikuta akilazimisha ile kauli ya abiria chunga mzigo wako, kutokana na kutompa mwandani wake, Najma Dattan ‘Naj’ nafasi ya kujiachia na watu wengine klabu na kugandana kama ruba.

barakah_daprince

Baraka na Najma

Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar kulipokuwa na shoo ya Usiku wa Pam D na Young D ndipo wasanii hao walitinga usiku mnene wakionekana kuwa beneti muda wote, hata pale mmoja wapo aliposalimiana na watu wengine hakumuachia mkono mwenzake kuhofia wajanja wangemshobokea.

Kutokana na ishu hiyo ambayo iliwafanya watu wabaki wakiwakodolea macho mwanzo mwisho, walipoulizwa waliishia kucheka na kudai kinachosababisha hali hiyo ni mahaba mazito waliyonayo.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364