-->

Rammy Galis Apata Shavu la Kuigiza Movie Mpya Nigeria

Muigizaji wa filamu nchini, Rammy Galis amepata shavu la kuigiza filamu mpya Nigeria iitwayo Her Shoes.

RAMMY44

Rammy alienda Lagos kumalizia kurekodi video yake iitwayo Red Flag lakini imebidi aendelee kuwepo huko baada ya kupata shavu la Nollywood.

“KAZI niliyo onesha #Maproducer wa Nollywood katika #RedFLAG hatimaye imeleta Matunda. #MUNGU Amepokea Dua zenu , Ameweza Kunipa Kazi Nyingine #HERSHOES HapaHapa Kabla Sijarudi Nyumbani #Tanzania na Kumbuka Hatua Moja Huanzisha Nyingine,” aliandika Galis kwenye Instagram.

RAMMY GILLS89

Kwenye picha nyingine, Galis aliandika: Baada ya Kusign Mkataba Leo kwaajil ya Kazi Mpya ya #HERSHOES Niliyo Tanguliza Script Yake , Nikiwa Na Director Nguli Wa Nollywood @sylvestermadu Ambaye Amesha fanya Kazi Nyingi, kushoto MV yke mpya akiwa na @ramseynouah #TheFamily… #MunguNisimamie.”

RAMMY90

Tayari wameshoot scenes kadhaa za filamu hiyo. Idris Sultan ni mmoja wa mastaa waliompongeza muigizaji huyo. “Napenda kuona actors wetu wanavuka mipaka kutangaza tasnia yetu. Big up bro @rammygalis icho kiingereza sio ishu, ishu hapo ni kazi so don’t loosed hope.”

Idris aliweka utani kwenye Kiingereza baada ya awali Galis kuandika caption kwenye picha yake iliyokuwa na tatizo la grammar ambayo tayari ameirekebisha.

Chini ni picha zingine za scenes za Her Shoes.

RAMMY GILLS23 RAMMY GILLS00

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364