-->

Barua ya Jack Cliff Yazua Simanzi Upya

Ikiwa imekatika miaka miwili tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, nchini China, Video Queen, Jack Cliff ameibua simanzi upya baada ya kuandika barua ya wazi kwa Watanzania.

Simanzi hiyo iliibuka mwanzoni mwa wiki hii mara baada ya barua hiyo kusomwa redioni na Mtangazaji Millard Ayo ambapo barua hiyo ilieleza kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwaweka sawa wanaosambaza taarifa za uongo zinazomhusu.

jack44

Katika barua hiyo, ameweka wazi kwamba anajuta kubeba madawa ya kulevya na mwisho wa siku kujikuta akiwa kwenye mikono ya polisi kitu ambacho hakukitegemea kabisa. Anahuzunika, ila pamoja na hayo yote, ameamua kuwaomba msamaha Watanzania wote kwa kile kilichotokea.
“Inasikikitisha, Mungu amsaidie atoke jamani maana kama kujuta ameshajuta vya kutosha,” alisema John Jimy, mkazi wa Mwenge Dar.

Huku taarifa zikiwa zimetolewa katika vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa mpenzi wake, Juma Jux na Mwanamuziki Vanessa Mdee ‘V Money’ katika barua hiyo, Jack amesema kwamba hawezi kuuzungumzia uhusiano huo ila kama Jux ana furaha katika mapenzi yake ya sasa, hiyo ndiyo furaha yake pia ila anamuomba msamaha kwa kumuumiza.

Ingawa taarifa zinasema kwamba watu wengi wamekuwa wakienda gerezani nchini humo kumuona lakini mwenyewe amesema familia yake ndiyo pekee ambayo imekuwa ikimjali na kumtembelea mara kwa mara.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364