-->

Bongo Muvi, TAFF Wamaliza Tofauti Zao

BIFU kubwa lililokuwepo kati ya wasanii wa fi lamu wanaounda Bongo Movie na wale wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘Taff ’ limeyeyuka baada ya viongozi wa pande zote mbili kukutana na kuona kuna ulazima wa kuwa kitu kimoja.

Jacob Stephan na Saimon Mwakifamba wakipeana mikono (2012)

Jacob Stephan na Saimon Mwakifamba wakipeana mikono (2012)

Taarifa za pande hizo mbili kumaliza tofauti zao zilitua kwenye dawati la gazeti hili na kuthibitishwa na Rais wa Taff , Simon Mwakifamba ambaye alisema wameona  aufanyie kazi msemo usemao Umoja ni Nguvu wakiamini wakiwa wamoja wanaweza kuleta maendeleo ya haraka.

“Ni kweli tulikutana na kuondoa tofauti zetu, lengo ni kuunda umoja madhubuti ili kuweza kuleta mafanikio ya haraka kwenye fi lamu kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano,” alisema Mwakifwamba.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364