Bulaya Sasa hamishiwa Bugando
Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime alikokimbizwa Jana Jumapili baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya polisi mjini Tarime, amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jjijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche amesema kuhamishiwa Bugando kwa mbunge huyo kumewezekana baada ya kupata dhamana ya polisi aliyowekewa na watu watatu akiwemo wakili wake, Alex Masaba.
Wengine waliomdhamini kwa kusaini hati ya Sh20 milioni ni Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko na Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele ‘B’, Pamba Chacha.
Heche amesema kabla ya kuachiwa kwa dhamana Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi (OCD), wa Tarime, Thomas Mapuli alimtembelea mbunge huyo hospitalini kuona hali yake kiafya.
Mwananchi