-->

Siwezi Kumuacha Ray – Johari

Msanii nguli wa filamu ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu Bi. Blandina Chagula, ameweka wazi mahusiano yake na muigizaji mwenzake Vicent Kigosi, ambaye wanamiliki kampuni moja ya filamu.

Akizungumza na mwandishi wetu Johari amesema hawezi kuvunja mahusiano yake na Ray ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji mwengine Chuchu Hansa, kwani wana miliki kampuni kwa pamoja.

“Mimi na Ray tunafanya kazi, kwa hiyo kuachana nae ni vigumu, naacaha nae kivipi sasa wakati wote tunamiliki kampuni ya RJ? Yule ni mkurugenzo mwenzangu kwa hiyo sio rahisi kuvunja uhusiano wetu”, alisema JOhari.

Pia Johari amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani anatarajia kuwapakulia kazi mpya, ambayo itakuwa inawaletea yule Johari waliyemzoea kwenye filamu zake zenye ubora wa hali ya juu.

“Unajua mi siwezi kuacha anaa kwa sababu sanaa ni maisha yangu, siku si nyingi ntatoa kazi mpya hii kazi haina kustaafu,m na sasa hivi wale wasanii wakongwe karibia wengi tunajipanga kurudi kwenye game, kwa hiyo watu wakae mkao wa kula”, alisema Johari.

Hivi sasa Johari amekuwa kimya kwa muda mrefu kuonekana kwenye kamera, na badala yake amekuwa mtu ambaye anakaa nyuma ya kamera kwenye utengenezaji wa filamu nyingi zinazotengenezwa na kampuni ya RJ.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364