-->

Calisah: Kama Sio Mimi ni Wema Aliyevujisha Video

Sinema ya model Calisah imezidi kushika kasi – amefunguka kwa kudai kuwa ni yeye au Wema Sepetu ndio waliovujisha video inaowaonesha wakilana denda.

wema-sepetu-1

Siku chache zilizopita mwanamitindo huyo wa kiume alikamatwa na polisi kwa kosa la kudaiwa kusambaza kipande hicho cha video lakini baadae aliachiwa.

Akiongea na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Calisah amesema, “Nilienda kwa Wema tukawa tunaongea vizuri tu najaribu kumuelezea, lakini hata yeye alishangaa kuona polisi wameingia. Si yeye ni wapambe wake ndio walienda kituoni, wabeba pochi tu, tena afadhali wangekuwa wanawake ni wanaume.”

“Picha zile tunazo mimi na yeye, kwa hiyo kama sio mimi niliyesambaza ni yeye na kama sio yeye ni mimi. Mimi sijasambaza siwezi kumdhalilisha mwanamke kiasi kile. Sasa hivi nampenda kama mshikaji kwa sababu tayari nina mwanamke mwingine ninayempenda,” ameongeza.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364