-->

Charugamba Ammwagia Sifa Rose Mhando

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Ussy Charugamba, amesema katika wakongwe kwenye tasnia hiyo, anamkubali zaidi Rose Mhando kwa kuwa amewaonyesha njia waimbaji wengi.

Rose Mhando

Bosi huyo wa Ussy Production, ameliambia MTANZANIA kuwa anajiona mwenye bahati kufanya kazi na Rose Mhando kwa kumshirikisha kwenye wimbo wake unaoitwa ‘Wema’ ambao utakuwa kwenye albamu yake ya sita.

“Rose Mhando ana mchango mkubwa kwenye tasnia hii, amefungua milango kwa waimbaji wengi kufanya hiki wanachokifanya sasa, binafsi najiona mwenye bahati na ninajivunia kufanya kazi na mkongwe huyu, naomba tumpe heshima yake,” alisema Charugamba.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364