Idriss Amuonea Huruma Sana Jack Wolper kwa Talaka za Mwezi Mwezi
MCHEKESHAJI na muigizaji wa filamu Bongo Idris Sultan amewaacha wapenzi wa filamu pale aliposema kuwa anamuonea huruma sana Jack Wolper kwa mikasa inayomkabili katika maisha yake ya mahusiano kwani amekuwa hana bahati kila mwanaume anayekutana naye lazima amuumize na hayo usimlimua akipigwa chini.
“Juzi hapa tumesikia kuwa alipata mwanaume akaenda kwake hana hela mama akajua mume kumbe dah! Naomba tumuombee apate mume anatia huruma sana kila mwanaume kwake ni majanga maskini Wolper,”
Idriss anasema kuwa amesikia kuwa Jack Wolper amepata mwanaume mwingine kwa sasa anatakiwa aombewe ili asimtende kama wale kwani Wolper hiyo ndio sehemu ya maisha yake kuwa na wanaume ambao uwatangaza kisha kulia baada ya kutendwa, na hayo usimulia baada ya mwezi akishaachika.