Chid Benz Akanusha Kutoroka ‘Rehab’ Adai Kuruhusiwa
Msanii Chid Benz amekanusha taarifa zilizopo kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kuwa ametoroka rehab Bagamoyo, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya.
Akiongea na East Africa Radio Chid Benz amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.
“Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa”, alisema Chid Benz.
Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.
Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.
eatv.tv