-->

Diamond Achukua Taji la Lip Sync Africa ya MTV

Diamond Platnumz amechukua taji la kipindi cha Lip Sync Africa kinachorushwa na kituo cha MTV SA.

DIAMOND13

D’Banj ambaye ni host wa show hiyo akimpongeza Diamond kwa ushindi

Alikuwa akichuana na mshkaji wake, Theo wa kundi la Mafikizolo. Kwenye kipindi hicho, wasanii wawili hushindana kuziimba nyimbo za wasanii wengine kwa kugandamizia na kupatikana mshindi mmoja.

Baada ya kuchukua ushindi huo na kupewa mkanda wake, Diamond aliandika kwenye Instagram: Ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuwajuza kuwa kijana wenu nimewawakilisha vyema kwenye mashindano ya LIP SYNC BATTLE AFRICA ya @MtvBaseAfrica na kuweza kuibuka kidedea kwenye Mashindano ya Stage hiyo na kunyakua Mkanda.”

Lip Sync Battle ni show iliyoanzia Marekani na kuongozwa na rapper LL Cool J na mke wa John Legend, Chrissy Teigen. Kwa Afrika show hiyo inaongozwa na mrembo wa Afrika Kusini Pearl Thusi na staa wa Nigeria, D’Banj.

Bongo 5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364