-->

Chuchu Azungumzia ‘Usaliti’

Mmoja wa waandaaji wa tamthilia mpya ya Usaliti Chuchu Hansi ameeleza kuwa tamthilia hiyo itaanza kuruka Jumanne ya leo saa 09:30 usiku kupitia EATV. chuchu amesema tamthilia hiyo itahusu migogoro ya kimapenzi na usaliti.

chuchu565
Chuchu amesema tamthilia hiyo itahusisha wakali kibao wa zamani na wa sasa akiwemo yeye mwenyewe na wengine kama Nyamayao, Thea, Senga na wengine kibao.
Kwa kiasi kikubwa vile vichwa vingi vya kundi la Kaole vitahusika. Pia Chuchu amesema anaamini vichwa vilivyohusika vitatoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa tamthilia za bongo.
Tamthilia hii itaonesha hali halisi ya usaliti wa kimapenzi katika jamii zetu ikiwa na lengo la kuelimisha zaidi.
Zaidi Chuchu alidokeza kuwa tamthilia hiyo imeandaliwa kisasa zaidi na itakuwa na ubora wa juu kuliko tamthilia nyingi za Bongo.

 

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364