Dada Zangu wa Bongo Movies Washobokaji Kasoro Riyama na Monalisa-NIVA
Staa wa Bongo Movie, Niva amefunguka na kudai kuwa dada zake wengi wa Bongo Movies wanapenda kuwashobokea wanaume hasa wakiona vitu kama magari.
‘Dada zangu wa bongo movies wengi washobokaji, watu ambao sio washobokaji ni wawili tu kwenye bongo movies nzima, Riyama na Monalisa kwisha, walionbaki wote ni washobokaji, wakimuona mtu hivi basi, shobo shobo”.
Niva alieleza hayo alipokuwa akihojiwa na soudy brown wa ‘Uheard’ kuhusu mashari tata aliyoitoa msanii Nay wa Mitego kuhusu wasanii wa Bongo Movies ambayo Niva ni moja ya wasanii wa Bongo Movies waliotajwa moja kwa moja kwenye mistari hiyo.
“…Kuna Nivar super Marioo ana Gari la Milioni Kumi ajawai ata miliki Getto, anaishi kwa Mademu wakiachana Gari ndio Geto.”- sehemu ya mistari ya Nay.
Niva alikanusha madai hayo kwa kueleza ana mjengo hapa mjini na Nay anajua kiasi cha pesa nachotengeneza kupitia kazi zake za sanaa na biashara.
Mbali na wanasheria wengi kumfata niva ili wamfungulie mashtaka Nay, Niva alisistiza kuwa Nay ni mdogo wake na wamesoma pamoja kwahiyo hawezi kumfanyia chochote kibaya.