-->

Davina: Naanzaje Kwenda kwa Sangoma kwa Mfano?

Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya ‘Davina’ juzikati alimjia juu mmoja wa mashabiki wake aliye-comment kwenye ukurasa wa msanii huyo wa Instagram kuwa alimuona akiingia kwa mganga wa kienyeji maeneo ya Kawe jijini Dar.

Davina

Davina

Davina alisema, amejikuta akiumia sana kwani yeye si mtu wa mambo hayo huku akihoji anaanzaje kwenda kwa sangoma wakati imani yake haimruhusu?
Akizungumza na Ijumaa juzi, Davina alisema shabiki yule hana adabu na akimjua atamshikisha adabu. “Siku hiyo nilifika maeneo ya kwa mchungaji mmoja aitwaye Elia pale Kawe kuwapeleka wasanii wenzangu walioniomba lifti baada ya kutoka lokesheni, sasa yule mtu anasema eti aliniona naingia kwa mganga, kaniudhi kweli,” alisema Davina.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364