Sijawahi Kutoka na Nisha -Baraka de Prince
Msanii Baraka de Prince ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake ya ‘SIWEZI’ na ambaye amedondoka kwenye penzi la msanii mwenzake Najma Datan amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake yeye hajawaji kutoka kimapenzi na msanii wa filamu nchini Salma Jabu alimaarufu kama ‘Nisha’.
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Baraka de Prince alisema kwamba yeye hajawahi hata kuwa na ushikaji na msanii huyo na kusema kwamba inawezekana ni shabiki mzuri wa kazi zake ila hajawahi kutoka nae kimapenzi kama ambavyo inazungumzwa mtaani na kama ambavyo msanii huyo alivyowahi kusema kuwa anatoka na Baraka de Prince.
Mbali na hilo Baraka de Prince alizungumzia juu ya show kubwa ambayo ataifanya siku ya kesho Jumapili pale Coco Beach kwenye show iliyoandaliwa na East Africa Radio kwa ajili ya kushererekea miaka 17 toka imeanzishwa. Ambapo Baraka de Prince amesema ni show yake ya kwanza kubwa kufanya hivyo amejipanda kuwapagawisha wana ambao watatokea,
“Unajua mimi ni msanii wa mtaani na watu wangu wengi wa mtaani huwa wanashindwa kuibuka kwenye show zetu hizi za Club na sehemu zingine ila naamini show ya kesho wataibuka wengi halafu mimi nitaimba nao mwanzo mwisho, sababu mimi ni mtu wao”.