Davina: Nimezaa Sijazeeka na Bado Nalipa
Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amedai kuwa kuzaa siyo kuzeeka kama wasanii wengine wanavyodhani bali ni kupata heshima na kupendeza kama alivyonawiri yeye.
Akizungumza na Ijumaa, Davina alisema kuwa yeye ni mama wa watoto lakini kila kukicha anazidi kupendeza na kuonekana ‘kigori’ tofauti na watu wanavyodhani.
“Unajua kuna baadhi ya watu wanadiriki hata kutoa mimba kwa sababu tu wasizeeke kwa kuzaa lakini wanaikosa furaha ya kuitwa mama, mimi napendeza kwa sababu sina stress, watoto wangu ndiyo kila kitu,” alisema Davina.
Chanzo: GPL