-->

Diamond Afunguka Kutotokea Kwenye Zari All White Party, Adai Hamwogopi Ivan

Diamond Platnumz alikuwepo, Kampala, Uganda usiku ambao Zari alikuwa akifanya party yake ya All White lakini hakutokea. Ex wa Zari, Ivan Ssemwanga na wapambe wake walikuwepo. Watu walihisi kuwa Diamond aliogopa kwenda kumpa kampani mama wa mtoto wake Tiffah ili kuepusha shari na kambi ya Rich Gang ya Ivan.

Diamond Akiwa na Zari

Diamond Akiwa na Zari

Hata hivyo muimbaji huyo wa Utanipenda amedai kuwa hakukacha party hiyo bali makubaliano aliyokuwa nayo na promota wa show yake ya Ijumaa (siku moja baada ya all white party) yalimtaka asiende kwenye show hiyo ili kutengeneza uspesho kwenye show yake na Patoranking na sio ukweli kuwa alimgwaya Ivan.

“Halafu sasa watu wanasema namuogoa [Ivan], mimi siwezi kumuogopa, hii code chafu kabisa kutoka Tandale mimi nimuogope mtu!,” alisema kwenye mahojiano ya jana kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Diamond amesema ameshawahi kukutana na Ivan mara kibao japo walipigiana mikausho kama kawa!

“Sijawahi kuwa na matatizo naye, nshakutana naye wakati naenda kwenye MTV alikuwepo, mara nyingi tulikuwa tunapishana hivi na hivi kabisa. Hatujawahi kusalimiana sababu sijawahi kuwa na mahusiano naye niseme nimsalimie ni uongo. Halafu nilikuwa nikipita, nipo na crew, security, yeye anakuwa anapita tu maskini ya Mungu.”

Chanzo: Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364