Filamu ya ‘Going Bongo’ Mzuka
ILE Filamu kubwa ya Going Bongo imepokelewa vizuri na wapenzi wa filamu kwa kukusanya watu wengi wakiwemo wasanii nyota kutoka viunga vya Bongo sinema hiyo ambayo imerekodiwa katika kiwango cha kimataifa ilirushwa katika ukumbi wa sinema wa Cinemax Mlimani City na kuteka watazamaji.
Mmoja wa wasanii nyota katika vichekesho Masanja Mkandamizaji alisifia ubora wa sinema hiyo na kusema sasa Tanzania imepiga hatua katika utengenezaji wa filamu na kitu muhimu kwa sasa ni kujipanga katika utunzi wa hadithi ili kupambana na sinema kutoka Hollywood na sehemu mahiri kwa utengenezaji wa filamu.
“Kiukweli sinema ni nzuri sana imetulia sauti safi picha kali wasanii wameigizaji katika kiwango cha hali ya juu sana hivyo ni changamoto kwa watayarishaji wa Bongo movie,”anasema Masanja.
Sinema ya Going Bongo imekuwa ikifanya vizuri na kuweza kujishindia tuzo kutoka katika matamasha mbalimbali ya filamu, sinema hiyo imerekodiwa Bongo na Amerika.
FC