-->

Dimpoz amwaga ugali ishu ya ‘Malkia wa Nguvu’, Je ni diss kwa Diamond?

Wiki hii rapa, Fid Q kaachia wimbo wake mpya ‘Fresh’ akiwa amemshirikisha Diamond pamoja na Rayvanny ambao umeibua mgongano mkubwa wa mawazo kupitia mitandao ya kijamii kutokana na mistari ya Diamond ambayo ilidaiwa kwenda kwa Alikiba.

Mkali huyo wa Aje alishindwa kuvumilia baadhi ya vitu vilivyozungumzwa katika wimbo huo na kuamua kunyesha mvua ya tweets ambazo zilidaiwa moja kwa moja kwamba amemjibu Diamond kupitia wimbo huo.

Hata hivyo Diamond alirudi tena na verse mpya kupitia beat ya wimbo huo huku akidaiwa kumchana Alikiba pamoja Ommy Dimpoz.

Verse zinazodaiwa kumgusa Ommy Dimpoz ‘Kufanya verse moja tu naona povu linawashuka, kina dada wavaa vi-top na vibukta/ Hawatoi ngoma kazi twiter kunisuta, kusafiria nyota nawapa pia na jua ruksa/ Wengine vishavu nukata, hips kama tuta, najiuliza ni nani au wameumbwa na hulka/Wapo pamoja post sina mafuta, msiniletee nuksi huwa silagi vipusa’

Jumatano hii Ommy Dimpoz amedaiwa kujibu mapigo, ingawa ni mafumbo lakini wadau wa mambo wanadai dongo hilo moja kwa moja lianaenda kwa Diamond.

Ommy ambaye kwa sasa ni msanii wa RockStar400, amepost picha akiwa na mama Diamond katika mtandao wake wa Instagram na kuandika ujumbe huu.

BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU

Salam zako nimezipata mwanangu Hivi kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa langu mimi nini???? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?
#UnanioneaKwaKuaSijuiKurap?
#SijuiNaMimiNimkatae??
#KamaYeyeAlivyomkataaWaMobeto
#YaniUnamkataaMjukuuWangu??
#UnakubaliKuleaWatotoWa5SioWako
#UmerogwaWWSioBureMwanangu
#NilikuwaNajuaNimezaaSIMBA
#KumbeNimezaaKIMBA
#DavidoNaeAnalalamiKuhusuENEKA
#UmeletaJanjaJanjaKwenyeFallOnU
#NnaedhalilikaMimiBabaYaKo??
#UtakujaKuniuaKwaPreshaJomoniiii?
#HayaNendaKatungeVesiNyingine?
#RahaYaVitaUsichagueSilaha
#BABAMALKIA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364