Dj Fetty Afunguka Kuhusu Kurudi Clouds FM
Dj Fetty ni mmoja kati ya watangazaji waliyoifanya mioyo ya wapenzi wa radio iwe na huzuni wakati wote tangu alipotangaza kuacha kazi hiyo mwezi Septemba mwaka jana kutokana na swagga zake anapokuwa kwenye kipaza.
Hakika mashabiki wa kipindi cha XXL cha Clouds FM ndio waliumizwa sana kwa wakati huo na mpaka sasa kutokana na kipindi hicho kupungukiwa kachumbari aliyokuwa nayo mtangazaji huyo.
Wiki hii mashabiki wa kituo hicho cha redio wameweza kupata faraja kidogo baada ya kuonekanana kwa kipande cha video kinachomuonesha mwanadada huyo akiwa kwenye ofisi za radio hiyo akisema kuwa anaweza kurudi mjengoni lakini atasikika kwenye kipindi kingine.
“I missed him. Kama unataka nirudi Clouds narudi Jahazi,” alisema Dj Fetty akiwa na Gadner G Habash.
Baada ya kauli hiyo Gadner ambaye ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho cha Jahazi alipigilia msumari kwenye mfupa kwa kusema, “Naongea naye, atakuwa ndiyo mtangazaji namba moja anayelipwa hela nyingi nchi nzima.”
Je ni kweli mwanadada huyo anaweza kurudi kwenye kazi hiyo?
Bongo5