-->

Dude Afunguka ‘Kumpiga’ JB

Mwigizaji Kulwa Kikumba maarufu zaidi kama Dude amefunguka na kudai ameshawahi kumuingiza mjini msanii mwenzake Jacob Stepheni (JB) kwa kumtapeli laki moja na thelathini japokuwa mwenyewe alifahamu.

Dude ameeleza hayo kwenye Big Chawa ndani ya kipindi cha Planet Bongo ya East Afrika Radio baada ya kuulizwa ni msanii gani amekaa kizembe zembe ambaye anaweza akatapeliwa kiurahisi.

“JB si unamuona amekaa kupigwa pigwa hivi, anachelewa kukumbuka kwanza mimi nimeshawahi kumpiga kiukweli kabisa kama shilingi laki 1 na thelathini. Anajua JB lakini alitoa kwa sababu mimi ni ndugu yake pia ni rafiki yake”, alisema Dude.

Pamoja na hayo, Dude aliendelea kwa kusema “JB ni mtu mmoja poa sana yani yule unaweza kumuingia wakati wowote ule ukiwa na shida za haraka haraka ukimdanganya tu umemuingiza mkenge”.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364