-->

Msanii Radio afariki dunia

Uganda. Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Moses Ssekibogo maarufu Radio amefariki dunia jana  alhamisi saa sita asubuhi.

Mwandaaji wa matamasha, Balaam Barugahara alimthibitishia mwandishi wa Dailly Monitor kuwa msanii huyo alifariki wakati akiendelea na matibabu hospitalini.

Msanii huyo ambaye alikuwa akifanya vizuri na mwenzie Weasel, tangu Januari 23 mwaka huu hali yake ilikuwa mbaya kutokana na majereha aliyoyapata kwenye ugomvi klabu ya De Bar kisha kupelekewa jijini Entbebbe kwa matibabu zaidi.

Rais wa Uganda, Yoweri Museven alitoa Sh30 milioni jana Jumatano kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo.

Pia kulikuwa na maombi maalumu yalikuwa yameandaliwa kwa ajili ya kumuombea ambayo yalitarajiwa kufanyika Februari 4 mwaka huu katika Kanisa la Light the World.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364