Dully Sykes Amgaragaza T.I.D
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, amemgaragaza Khalid Mohamed ‘T.I.D’ kwa idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wao.
Wasanii hao walishindanishwa katika kituo cha radio One ambapo walikuwa wanawashindanisha kwa ubora wa nyimbo zao huku mashabiki wa muziki huo wakipiga kura kumchagua mkali zaidi.
Dully alifanikiwa kuibuka kidedea kwa kumzidi mpinzani wake kwa kura 12-11 za mashabiki ambao walifuatilia shoo hiyo.
Nyimbo ambazo zilimpa ushindi Dully ni pamoja na ‘Hai’ na ‘Dhahabu, huku nyimbo za T.I.D zikiwa ni ‘Understanding na ‘Mpenzi Lisa’.
Mtanzania