-->

Irene Uwoya: Mwanamke Anastahili Heshima

MSANII wa filamu nchini, Irene Uwoya, amesema mwanamke anastahili heshima ya hali ya juu kwani amekuwa ni nguzo ya familia na mafanikio katika jamii inayomzunguka.

Irene Uwoya Katika Pozi

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema katika kila familia iliyoweza kupata mafanikio, lazima mwanamke atakuwa amehusika.

Alisema kwenye maisha yake amekuwa akifanya kazi kwa nguvu zote bila ya kujali kuwa yeye ni mwanamke na anaamini jinsia haiwezi kumzuia mtu kuongoza sehemu yoyote.

“Mfano mdogo ni mimi nilipoamua kujikita katika siasa mwaka 2015, nilipitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Vijana Mkoa wa Tabora, niliweza kujikubali na kujaribu ingawa sikufanikiwa.

Alisema baada ya uchaguzi kupita, aliendelea na majukumu yake ya kawaida katika maisha kwa kuelimisha wanawake na wadada juu ya mwonekano wa mavazi na kufungua duka la nguo lililopo Msasani jijini hapa.

“Njia ya kupambana na maisha, niliamua kufungua duka la nguo ambapo ninauza nguo za wanawake na wadada ili kuonyesha jinsi gani wanaweza kuongeza mwonekano wao.

Irene alisema hivi sasa ni mlezi wa chama cha wanawake ambacho kinaitwa ‘Mwendokasi’, kilichoanzishwa kwa lengo la kusaidia wanawake kuazisha vikoba endelevu na ameweza kuchagia milioni 3 ili kutunisha mfuko wa chama hicho.

Alieleza kuwa ni vema wanawake wakajituma na kufanya kazi kwa bidii, kwani hakuna kinachoshindikana kama watakuwa wabunifu.

“Serikali inatakiwa kusaidia wanawake kwa kuwapa mikopo ya gharama nafuu ili waweze kuendesha biashara zao ndogo ndogo, kwani nimejifunza mengi kupitia ya sanaa pia wanawake tunaweza kuishi bila ya kutegemea mwanamume kama tunaonyesha juhudi na kuthamini kile tukifanyacho,” alisema Uwoya.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364