-->

Erick Omondi Amsapoti Nishabebee Kuuza Filamu ya Kiboko Kabisa

Erick Omondi akiwa na Nishabebee

UNAPOTAJA jina la Erick Omondi ni jina kubwa kwa sasa barani Afrika kijana mdogo mahiri katika uchekeshaji mwenye sifa kubwa Afrika ya Mashariki, msanii huyu ni bingwa wa kutawala jukwaa, alikuja Dar es salaam kwa show maalum na kuamua kumsapoti Nishabebee kuuza filamu ya Kiboko Kabisa.

“Mimi natamba sana na stage but Nisha ni Kiboko kabisa katika kuact filamu na anafuns wengi hata kwa Kenya so naungana naye katika kuhakikisha anauza filamu ya Kiboko kabisa na kuwa Plutnamu mauzo ya juu kabisa,”anasema Eric

nisha -eric omond

Meneja wa Nishabebee Myovela akiwa na Erick Omondi na Nishabebee katika kikao Holiday Hotel

Wiki hii msanii huyo katika kumsapoti msanii mwenzake kutoka Swahilihood Nishabebee aliipigia debe filamu hiyo kwa kuwashawishi wapenzi wa filamu wainunue kwa sababu anamjua vizuri Nisha kwa kazi bora na watafurahi bila kujutia pesa zao.

Filamu ya Kiboko kabisa ipo madukani nchi nzima na inapatika katika maduka yote ya filamu Bongo , ni sinema ya kipekee kufanyika Bongo ikiwashirikisha wasanii kama King Majuto, Mzee Jengua, Ben Blanko, Nishabebee na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu Bongo.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364