-->

JB Ataka Kuwa wa Kimataifa

jb23

MKALI wa Filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’ amefunguka kuwa ameamua kuja kivingine katika tasnia ya filamu mwaka huu kwa kuiboresha zaidi kwa kushirikiana na wasanii kutoka nchi mbalimbali ili kuweza kutusua kimataifa.

Akizungumza na Mikito Jumatano, JB alisema, licha ya filamu zake kadhaa alizoziachia huko nyuma kufanya vizuri, pia yupo katika mikakati madhubuti ya kuandaa filamu nyingine lukuki.

“Kuna filamu nimetoa Desemba, mwaka jana, lakini kwa sasa nipo katika harakati za kutoa filamu mpya inayoitwa Kalamba Tirobo, filamu hii nitamshirikisha Dayana Kimaro ambayo ni ya kitapeli ikiwa ni muendelezo wa filamu zangu za utapeli ambazo nyingine ni Kinecha, Bachela na Mzee wa Swaga ambayo itatoka Machi, mwaka huu nikiwa nimemshirikisha Majuto.

“Filamu nyingine ninazotarajia kuzifanya ni ya Karata Tatu ambayo nitawashirikisha wasanii ambao wana majina lakini hawachezi sana filamu kama Thea, Bi Hindu na wengineo.

“Lakini ukiacha hivyo nafikiriia kufanya tamthilia nyingine nzuri ya kuwashirikisha wasanii kutoka nchi tatu, Tanzania, Zambia na nchi nyingine ambayo bado naendelea kufanya mazungumzo na wasanii wengine ambao nitawaweka wazi baadaye,” alisema JB

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364