-->

Faiza Aonya Mastaa Kuibiana Mabwana

MREMBO ambaye jina lake lilivuma zaidi baada ya kutinga na ‘pampers’ kwenye sherehe yake ya kuzaliwa, Faiza Ally, amewaonya mastaa wenzake kuacha kutafuta umaarufu (kiki) kwa kuibiana mabwana.

FAIZA ALLY42

Akizungumza na mwandishi wetu, Faiza ambaye ni mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, alisema anatambua mastaa wengi ustaa wao hauji kwa kufanya kitu fulani muhimu kwenye jamii kitu ambacho si sahihi.

“Mastaa wengi Bongo kiki zao zinakuwa si nzuri kwa sababu wengi wanatafuta kiki kwa njia ya kukwapua bwana wa watu sasa mwisho wa siku utajikuta ushamaliza mabwana wote utafanya nini? Mimi naona kiki kama hizo siyo nzuri kabisa katika jamii, waache,” alisema Faiza ambaye amejiingiza kwenye gemu la filamu na kurekodi filamu ya Baby Mama Drama.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364