-->

JB: Ugumu wa Soko la Filamu Umenibadilisha

JACOB Stephen ‘JB’ anasema kuwa ugumu wa soko la filamu umemfanya aangalie njia nyingine ya kufanya sanaa yake iendelee kuwa bora kwa kuanza kurekodi tamthilia tofauti na awali alijiwekeza sana katika Filamu pekee kwani lengo ni kufikisha ujumbe kwa jamii.

JB8990

“Dunia inabadilika na inaenda kwa kasi sana hivyo ni lazima pia mtu ubadilike, kazi ya filamu ni ngumu na inachangamoto zake hasa suala la soko kuliko kupoteza muda na kutokuwa na uhakika wa soko bora niingie katika tamthilia,”anasema JB.

JB ni moja kati ya wasanii wakongwe na bora kabisa katika tasnia ya filamu  ambaye siku zote amekuwa akifanya vizuri sana na sasa anageukia tamthilia huku akisema kuwa amejipanga kutoa ajira kwa wasanii chipukizi wengi tofauti na anapotengeneza filamu utumia wasanii wachache.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364