-->

Filamu ya Tanzania Kuonyeshwa Tamasha la Marekani

BAADA ya mafanikio makubwa iliyopata filamu ya ‘Aisha’ ilipoonyeshwa kumbi mbalimbali ikiwemo Nafasi Artspace na Pangani, filamu hiyo imechaguliwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la filamu la New African Films litakalofanyika Washington D.C. nchini Marekani, mwaka huu.

Aisha-film

Pia filamu hiyo imechaguliwa kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la filamu duniani katika maeneo manne mashuhuri ambayo ni Los Angeles, Toronto, New York na Singapore.

Ratiba ya maonyesho hayo kwa filamu hiyo ni kama ifuatavyo, Toronto, Canada itaonyeshwa Septemba 23 hadi 29, Singapore itaonyeshwa Septemba 30 hadi Oktoba 6, Los Angeles, Marekani itaonyeshwa Oktoba 14 hadi 20 na New York, Marekani itaonyeshwa Oktoba 21 hadi 28.

Filamu hiyo pia imeendelea kupata neema baada ya kuchaguliwa katika tamasha la kimataifa la filamu la ‘Seattle’ ambalo litakuwa likiadhimisha miaka yake 42 tangu kuanzishwa kwake.

Tamasha hilo litafanyika Mei19 hadi Juni 12, ni tamasha kubwa linalohudhuriwa na watu wengi nchini Marekani ambapo filamu takribani 400 kutoka nchi 80 zitaonyeshwa katika tamasha hilo linalodaiwa kuwa kubwa zaidi Amerika Kusini.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364