Rais wa Shirikisho la Filamu Asema Haya Kuhusu Janga la Madawa ya Kulevya Kwenye Tasnia
Baada miaka ya hivi karibuni kuibuka kwa wasanii wengi wa muziki kuhusishwa na matumizi ya Madawa ya kulevya, Rais wa Shirikisho la Filamu ‘TAFF’ Simon Mwakifwamba wamewapongeza wasanii wa filamu kwa kutokujihusisha na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Akizungumza na Clouds FM Jumanne hii, Mwakifwamba amesema kuwa hakuna msanii wa tasnia hiyo anajihusisha na utumiaji wala uuzaji wa madawa hayo.
“Sisi kwa upande wa filamu hatuna watumiaji wa madawa ya kulevya kama ilivyo kwa wasanii wa muziki wao ndio mara nyingi wanaathirika na suala hilo la madawa ya kulevya sijawahi kusikia wala kupata taarifa au ushahidi wa kutosha kwamba kuna wasanii wanafanya biashara hiyo ya ‘unga’, alisema Mwakifwamba.
“Inategemeana na wasanii wenyewe kwa sababu tunaona wasanii wengi wana siri zao,kuna wengine wanasema hawawezi kuimba bila kuvuta bangi,hivyo ni vilevi leo unaanza bangi kesho unaanza kutumia unga,lakini lingine ni suala zima la kuiga sana ‘umagharibi’. Lakini suala lingine ni njaa labda muziki haulipi hajapata show na kushawishika kufanya biashara hiyo. Kitu kingine ni kupenda maisha ya ‘shortcut’ kwamba akifanya hivyo atapata pesa kwahiyo anaanza kubeba mwisho unajikuta unatumia’’ aliongeza Mwakifwamba.
Pia Mwakifamba alisema anawashauri wasanii wa filamu kuendelee kuwa na rekodi nzuri ya kutotumia madawa ya kulevya kwasababu wao ni nguvu kazi ya Taifa.
Bongo5