-->

‘Fisi’ Aliyefanya Ngono na Watoto Malawi Akamatwa

Raia mmoja wa Malawi alionekana katika habari moja ya BBC akihusishwa na tambiko la usafishaji wa wasichana wadogo kupitia kushiriki ngono nao amekamatwa.

mzee4

Aniva

Eric Aniva amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu ya rais Bright Molande aliyezungumza na BBC.

Amesema kuwa Bw. Aniva aliyepewa jina la utani kuwa ‘fisi’ kwa jukumu lake katika uovu huo atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.

Pia amesema kuwa rais amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo.

Mtu aliyetajwa katika habari hiyo ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100 pia imebainika kuwa alikuwa na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

Tamaduni hiyo ya usafishaji ilipendekezwa na kufadhiliwa na baadhi ya jamii kusini mwa Malawi lakini serikali imejaribu kuisitisha.

BBCSWAHILI

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364